Thursday, December 8, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 99 & 100 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Read More
==

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 8

Read More
==

Wednesday, December 7, 2016

Waziri Mkuu Majaliwa aibana NCAA, ataka nyaraka za Faru John ifikapo Desemba 8, 2016

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameugiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro (NCAA), kumpelekea nyaraka zote zilizotumika katika kumhamisha faru maarufu kwa jina la John katika hifadhi hiyo ifikapo Desemba 8, 2016.

Majaliwa amesema ana taarifa kuwa walimhamisha Faru John Kreta kwa siri na kumpeleka  V I P Grumet  Serengeti Disemba 17, 2015 na waliahidiwa kupewa sh. milioni 200 ambapo  na wamepewa sh.  milioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa sh. milioni 100 nyingine baadaye.

Amesema hayo Desemba 6, 2016 alipotembelea Ofisi za makao makuu ya NCAA, zilizoko wilayani Ngorongoro mkoa Arusha  wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa  Baraza la Wafugaji ikiwa ni  sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

“Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,”.

Aidha, Majaliwa amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo ambao wanawakabidhi watoto kupeleka ng’ombe wao ndani ya kreta. “ Watumishi wa Ngorongoro ndiyo wanaopeleka ng’ombe ndani ya kreta na si wenyeji. Sasa marufuku na tutakayemkuta hatutakuwa na msamaha naye,”.

Amewataka watumishi hao kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wanafanyakazi kwa kufuata misingi ya kiutumishi na kuacha tabia za kuendekeza rushwa na wizi.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili na tayari  anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

“Haiwezekani mtumishi  awe anachunguzwa  na TAKUKURU halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini,” alisema.
Read More
==

Isikilize Video ya Rais Magufuli Akiwapiga Marufuku Wakuu wa Mikoa Kuwasumbua Machinga


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.
 
Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo  tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.
Read More
==

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 49 & 50 (Mwisho)Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
Read More
==

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Disemba 7

Read More
==

Tuesday, December 6, 2016

Waziri Mkuu aagiza pampu za maji kuondolewa kwenye chanzo cha maji Karatu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi. Theresia Mahongo kuhakikisha mashine zote za kupampu maji zilizoko ndani ya mita 500 kutoka kwenye chanzo cha maji cha Qangded ziwe zimeondolewa ifikapo saa 12.00 jioni ya jana na atakayekaidi atachukuliwe hatua za kisheria.

Alisema kitendo cha kuweka mashine za kupampu maji karibu na chanzo hicho na kuvuta maji kwenda kwenye mashamba yao kinasababisha maji kushindwa kufika katika mashamba ya wakulima wengine hivyo amewataka wafuate utaratibu uliowekwa na waendeshaji wa mradi huo.

Waziri Mkuu alitoa agizo jana Jumatatu, Desemba 5, 2016 wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Jobaji kata ya Baray wilayani Karatu, ambapo alisema Serikali haitavumilia kuona mtu mmoja akivuruga mradi huo wa umwagiliaji.

Alisema ili kuhakikisha mradi huo wa umwagiliaji unakuwa endelevu lazima chanzo cha maji kilindwe na wananchi wasiruhusiwe kufanya shughuli za kijamii karibu na chanzo na badala yake wasogee umbali wa mita 500.

“Sitaki kuona mashine zikipampu maji ndani ya mita 500 kutoka kwenye chanzo na badala yake wakulima wote wafuate taratibu zilizowekwa . Lazima chanzo kilindwe kwa sababu maji yakikauka mazao nayo yatakauka, hivyo tutakosa chakula jambo ambalo hatutaki litokee. Mkuu wa wilaya kesho nenda kafanye ukaguzi katika chanzo ukikuta mashine kamata,” alisema.

Awali, Waziri Mkuu alizindua mradi wa maji safi na salama wa kijiji cha Jobaj unaotekelezwa na shirika la World Vision Tanzania uliogharimu sh. milioni 285. Mradi huo utahudumia vijiji vitatu vya Kata ya Baray ambavyo ni Mbunga Nyekundu, Jobaj na Dumbechand.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Wolrld Vision Tanzania, Bw. Revocutus Kamara alisema mradi huo unatokana na hitaji kubwa la maji katika vijiji hivyo vitatu na uwepo wa kisima kirefu cha maji kilichochimbwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mwaka 2009.

“Mradi huu wa maji unatekelezwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ilianza Machi hadi Novemba 2016, ambapo wakazi 5,272 ikiwa ni pamoja na taasisi nne za Serikali ambazo ni Zahanati, Magereza, shule ya msingi na sekondari zilizoko katika kijiji cha Jobaj wananufaika kwa kupata maji safi na salama,” alisema.

Alisema awamu ya pili na ya tatu ya mradi huo itaanza Disemba 2016 na itagharimu zaidi ya shilingi milioni 200.

Akizungumza kuhusu mradi wa umwagiliaji Mkurugenzi huyo alisema shirika lao limechangia kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga kilomita 1.716 za mfereji katika kijiji cha Jobaj (kilomita moja) na Dumbechand (mita 716) ambapo umegharimu zaidi ya sh. milioni 210 na inalenga kunufaisha zaidi ya wakulima 4,450 wa vijiji hivyo.

Alisema mifereji hiyo itawezesha wakulima katika vijiji hivyo kuwa uhakika wa upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa mazao ya chakula na biashara hivyo itasaidia kupunguza migogoro ya maji, kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 803 hadi hekta 1,203.
Read More
==

Rais Magufuli na mkewe Mama Janet wakabidhi msaada wa Sh mil 5 ya matibabu ya Mtoto anayeotwa na nyama kichwani


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli jana  tarehe 5 Desemba, 2016 wamekabidhi msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto Haidari Bonge mwenye umri wa miaka 9 anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama kichwani, kinywani na machoni.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Mama wa mtoto huyo Sauda Kassim  na Kaimu Mnikulu Ndugu Ngusa Samike kwa  niaba ya Rais Dokta Magufuli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mtoto huyo anapatiwa matibabu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo, Kaimu Mnikulu Ndugu Ngusa  Samike alisema Rais Dkt. Magufuli ameguswa baada ya kutazama kipengele cha Hadubini “Habari kwa Kina” kilichorushwa hewani katika taarifa ya habari saa 2 usiku na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) tarehe 03 Desemba, 2016.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya ngozi Dkt. Andrew Foi alisema mtoto Haidari anayeishi Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam alianza kuota nyama miezi mitatu baada ya kuzaliwa na amekuwa akifanyiwa upasuaji wa kuondoa nyama hizo mara kwa mara.

Dkt. Foi alisema Hospitali ya Taifa Muhimbili inatoa matibabu ya mtoto huyo bure tangu awasili hospitalini hapo isipokuwa kwa matibabu ambayo hayapatikani hospitalini hapo ndio analazimika kuyalipia katika sehemu husika.

Alisema mtoto Haidari anahitaji eneo maalum la kuishi muda wote ambalo lina giza na kuvaa nguo nyeusi zinazomfunika mwili wote ili kujikinga na miale ya jua ambayo imekuwa ikimuathiri kwa kiasi kikubwa.

Mama wa mtoto Haidari, Ndugu  Sauda Kassim alimshukuru Rais Dkt. Magufuli na mke wake Mama Janeth Magufuli kwa moyo wa upendo waliouonesha baada ya kuguswa na shida zinazomkabili mtoto wake na kutoa msaada huo na hivyo kuomba wananchi wengine waige mfano wa Rais na Mkewe katika kumsaidia mwanawe.

Tayari mtoto Haidari  Bonge, ameshafunguliwa akaunti katika Benki ya CRDB tawi la Azikiwe yenye namba 0152236450100, ambapo benki hiyo kupitia kwa meneja Uhusiano wake Godwin Semunyu amekabidhi shilingi laki Tano ikiwa ni msaada kutoka Benki hiyo.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Read More
==

Profesa Muhongo: Tuna nishati ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema Tanzania kwa sasa ina hazina ya kutosha ya makaa ya mawe na gesi itakayowawezesha wawekezaji kupata nishati ya uhakika.

Waziri Muhongo pia ameahidi kuendeleza mradi wa usambazaji umeme vijijini ili kutimiza lengo la kila mtanzania kuwa na uhakika wa kupata nishati ya umeme.

Profesa Muhongo amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kikanda wa masuala ya nishati endelevu uliwakutanisha washiriki kutoka nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Afrika.

Katika mkutano huo, Waziri Muhongo aliwataka wadau hao kutafuta suluhisho la upungufu wa nishati kwa kuzingatia malengo ya milenia yanayotaja nishati kama moja ya sababu za kuinua uchumi.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez alisema nchi za Afrika zinahitaji kutumia teknolojia, sera na uwezo walio nao katika kupambana na suala la upungufu wa nishati huku umoja huo ukiahidi kutumia jumla ya dola za Kimarekani bilioni mbili katika kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu.
Read More
==

Kipindupindu charejea kwa kasi, chatikisa mikoa 6


Serikali imesema kumeibuka upya kwa ugonjwa wa kipindu pindu katika mikoa sita ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wapo wagonjwa 458 huku sita wakiwa wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu aliitaja mikoa yenye wagonjwa wa kipindipindu kuwa ni pamoja na Morogoro wagonjwa 282 na Dodoma wagonjwa 96.

Aliitaja mikoa mingine kuwa ni Mara wagonjwa 31, Kigoma wagonjwa 30, Arusha 11 na katika jiji la Dar es salaam wapo wagonjwa 8 wa kipindupindu kati ya hao 6 kutoka Ubungo na 2 kutoka Ilala.

Aidha, Mh. Waziri amebaini kuwepo kwa uzembe mkubwa unaofanyika katika wilaya na mikoa kwa kushindwa kutoa taarifa za ugonjwa huo huku wagonjwa wa kipindu pindu wakilazwa pamoja na wagonjwa wa kawaida kwa kile kinachoelezwa ni viongozi kuogopa kutumbuliwa na Rais Dkt. John Magufuli.
Read More
==

Ajali ya Lori na Hiace Yaua Watu 9 na Kujeruhi 18

Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace. 
Read More
==

TANZIA: Aliyekuwa mbunge wa Rufiji na daktari bingwa wa moyo, Prof. Mtulia afariki dunia

Profesa Idris Mtulia aliyefariki dunia jana, ameacha pengo katika sekta ya afya huku wagonjwa zaidi ya 20 wakimsubiri awafanyie upasuaji. 

Daktari wa Hospitali ya Tumaini, Profesa Chalonde Yongolo (aliyewahi kufanya kazi na Profesa Mtulia) alisema licha ya kuwa mwalimu wake, alikuwa akishirikiana naye kufanya kazi hospitalini hapo.

 Profesa Mtulia (pichani) aliyefariki dunia ghafla nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam jana asubuhi imeelezwa alikuwa mchapakazi, mwenye maadili msaada mkubwa kwa jamii.

“Ni pigo kubwa, leo alikuwa na wagonjwa 20 ambao walitarajia kupata huduma ya upasuaji. Nimepokea taarifa za msiba huu saa sita mchana na kwa mujibu wa mke wa marehemu kifo chake ni cha ghafla kwa kuwa aliamka salama na alipata kifungua kinywa na akaenda kupumzika na kupitiwa na mauti.” 

Profesa Mtulia aliwahi kuwa mbunge wa Rufiji na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD). 

Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema licha ya kuwa alikuwa amemaliza muda wake lakini Profesa Mtulia aliitumikia bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu. 

“Bado alikuwa mshauri katika mambo mbalimbali yahusuyo bodi.”
 
Bwanakunu alisema Profesa Mtulia alikuwa mchangamfu, mcheshi na huru kuzungumza na watu wote pasipo kujali rika. 

“Hakuwa mtu wa kawaida, alikuwa daktari hivyo alifanya majukumu yake kama mtu anayeelewa vizuri kitu anachokifanya na hata baada ya kumaliza muda wake mchango wake ulikuwa ni muhimu. 

"Alikuwa mtaalamu wa afya, msikivu na mpenda haki aliyehakikisha watu wanapata huduma kwa muda mwafaka."
Read More
==

Mali za Yusuf Manji Hatarini Kukamatwa, Kuuzwa


Siku moja baada ya mfanyabiashara Yusuf Manji kuhama kwenye jengo la Quality Plaza, uongozi wa kampuni ya udalali ya Yono umesema kinachosubiriwa ni mfanyabiashara huyo kulipa deni au kukamatwa kwa mali zake.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Stanley Kevela alisema Manji alipewa siku 14 zilizoanza kuhesabiwa tangu Jumamosi ili kulipa deni.

Alisema endapo siku hizo zitamalizika bila kulipwa, mali za mfanyabiashara huyo zitakamatwa ili kufidia deni la Dola 6.1 milioni za Marekani (zaidi ya Sh13 bilioni) anazodaiwa.

Kevela alisema fedha hizo ni gharama ya kupanga kwenye jengo hilo ambalo ni mali ya Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF).

Alisema baada ya kukamilika kwa mchakato huo, kampuni italikabidhi jengo hilo kwa PSPF kwa ajili ya shughuli nyingine.

Mfanyabiashara huyo alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mkononi haikupatikana.

Mkurugenzi wa kampuni ya Yono, Skolastika Kevela alisema kazi ya kuondoa mali za mpangaji kwenye jengo hilo ilikamilika juzi.

“Kampuni zote zimeshaondoa vifaa na milango ya jengo hilo imefungwa kwa kufuli za kampuni yetu. Tutalisimamia jengo hadi tutakapowakabidhi PSPF,” alisema.

Uamuzi wa Manji kuhamishwa kwenye jengo hilo ulitolewa na Mahakama kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango ambapo  alipewa masaa 24 ya kuondoa vitu  vyake.
Read More
==

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba 6

Read More
==

Monday, December 5, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Disemba 5

Read More
==

Sunday, December 4, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya Disemba 4

Read More
==

Saturday, December 3, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 97 & 98 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Read More
==