Sunday, August 5, 2012

AGNESS MASOGANGE: SINTAH NDO MTU ALIYESAMBAZA MKANDA WANGU WA XX
Mrembo 'Classic'  Agness Gerald 'Aggy Masogange' anayeng'arisha nyota yake kupitia viedo za wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, amemtupia zigo la lawama mwigizaji Christina Manongi 'Sintah' kufuatia kuvuja kwa mkanda wa video unaomuonyesha akiwa mtupu.

katika mahojiano aliyoyafanya na kituo kimoja cha redio Bongo, Aggy, amefunguka kuwa akiwa safarini nje ya Bongo alipewa taaraifa za kupotea kwa Digital Camera ambayo anadai ndiyo ilitumika kurekodia video hiyo na baada ya uchunguzi kufanywa na watu wake wa karibu iligundulika kuwa mwigizaji huyo ndiye anahusika na kupotea kwa kamera hiyo huku pia akidai ndiye aliyefanya kazi ya kusambaza video hiyo kwenye vyombo vya habari na mitandao kadhaa.

"Nilipewa taaraifa ya kupotea kwa kamera hiyo, nina hakika atakuwa sintah ndiye aliyefanya kazi ya kuisambaza, awali nilitaka kuchukua hatua juu ya jambo hilo lakini nikashauriwa na watu wangu kuwa nisifanye hivyo, kwa kweli najisikia vibaya lakini namwachia Mungu". alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!