Sunday, August 19, 2012

ALICHOSEMA BARNABA KUHUSU NAFASI ALIYOPATA KUMUANDIKIA 2FACE MISTARI.


.
Mwimbaji Barnaba atakua mwakilishi pekee wa Tanzania kupata mwaliko wa kwenda kuperform London U.K kwenye tamasha la wanamuziki mbalimbali wa nchi za Afrika ambao wanajitolea kuperform alafu zile pesa zinazopatikana zinarudi kwenye nchi zao kusaidia matatizo mbalimbali.

Kuhusu Barnaba kumuandikia mstari msanii 2face wa Nigeria, amesema “niko nae na nimepata bahati baada ya kutumiwa barua na wahusika kwamba nitaparform nae pamoja kwenye stage, katika vitu tutakavyofanya pamoja ni mimi kumuandikia chorus ya wimbo wake wa ‘African Queen’ kwa kiswahili aimbe na mimi nitaiimba chorus ya huo wimbo kwa kiingereza”

Mbali na 2Face, wasanii wengine watakaoperform kutoka Africa ni pamoja na D’banj na Mr Flavour na tamasha linafanyika London 27 August 2012 ambapo Barnaba anatarajia kuondoka siku yoyote kuanzia kesho.

Msikilize Barnaba akiimba akapela ya huo wimbo wa 2Face Idibia.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!