Wednesday, August 15, 2012

“AT” AAMUA KU-RAP NDANI YA NGOMA MPYA ‘TUNAFANYA MAMBO’


BAADA ya kuzoea kumuona kila wimbo anaotoa ni wa mduara sasa msanii wa miodoko hiyo nchini Ramadhan Ally ‘AT’, ameamua ku-Rap, katika ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Tunafanya mambo’, aliyoifanya na mtoto mmoja wa kizungu anayeishi nchini Sweden ingawa ni mtanzania.

Ku-rap kwa msanii huyo ndani ya ngoma hiyo kumekuja baada ya mtoto huyo kutaka kufanya kazi ya pamoja lakini awe ana Rap, hivyo anaamini watu watamuona tofauti kidogo ingawa kwa upande wake anaona muziki wowote anaweza kufanya.


Hata hivyo alisema kuwa video ya ngoma hiyo inaanza kupigwa picha kesho na wanahitaji audio na video ziweze kutoka kwa pamoja.


“Uwezi amini nimefanya ngoma ya Kurap na najua watu watu watanichukulia tofauti sana lakini najua uwezo wangu ni mkubwa katika kila aina ya muziki ninaotaka kufanya, na hii kazi itakuwa na uwezo wa kusikilizwa popote pale kutokana na uzuri wake,” alisema.


Hata hivyo aliongeza kuwa baada ya ngoma hiyo atakuwa katika maandalizi yake mengine ya kutoa kazi mpya, ambayo bado hajajua ipi itakayokwenda hewani kwani amefanya kazi mbili na wasanii mahiri wa taarubu moja na 
Hadija Kopa na nyingine na Mzee Yusuph.

“Kuna ngoma mbili ambazo sijajua ipi itaanza kwenda hewani hivyo nahitaji kukaa na wadau ili waweze kunishauri niitangulize ipi ingawa ngoma zote ni kali sana,”
alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!