Sunday, August 26, 2012

AVRIL WA KENYA ATAMANI KUFANYA NGOMA MOJA NA LINEX WA TANZANIA


Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya Avril Nyambura ambaye Jumapili hii atatua jijini Dar es salaam akiongozana na mwenzake Marya, amesema ana mpango wa kufanya wimbo na Linex.


Taarifa hiyo ameitoa jana alipoongea na E-News ya EATV.
“Kwa upande wa Tanzania tumekuwa tukizungumza naye Linex pia kuna wasanii wengine tumekuwa tukiwasiliana nayo huku na kule. So maybe tutapata time tuingie studio and see what we can do, we supposed to fly out on Monday afternoon,” alisema.

Hata hivyo Mpekuzi  imezungumza na Linex ambaye amesema Jumapili hii atakuwa mkoani Kigoma hivyo uwezekano wa kufanya ngoma na Avril kuwa mdogo.

Kuhusu show ya Jumapili hii jijini Dar es Salaam, Avril amesema ataperform wimbo wake mpya uitwao Kitu Kimoja.
“I hope nitaweza kuwafunza watanzania kuwa sisi sote ni kitu kimoja, East Africa.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!