Monday, August 27, 2012

BABY SHOWER: UTAMADUNU ULIOINGIA KWA KASI MJINI


Mama mtarajiwa akipata baraka kutoka kwa mashoga zake

Let me be honest. Leo ndio mara ya kwanza kuujua utamaduni huu uitwao ‘Baby Shower’. Nakubali kuwa mshamba kwa hili. Huenda wewe ni miongoni mwa watu kama mimi ambaye tulikuwa hatujui Baby Shower ni mdudu gani. Kama ulikuwa unafahamu, basi safi sana. Nimeufahamu vipi leo? Well ni kupitia ukurasa wa Miss Tanzania wa zamani Basilla Mwanukuzi. 

Nancy Sumari akiwa na mama mtarajiwa
Nilikuwa nikiona akishare picha nyingi zinazowaonesha wanawake wakiwa na nguo nyeupe na wawili wakiwa wajawazito. Katika picha hizo nikaona sura za watu wengi maarufu kama Nancy Sumari, Flaviana Matata, Mwamvita Makamba na wengine.


\
Katika Baby Shower hupikwa chakula cha kawaida
Nikaingiwa na udadisi ili kutaka kujua nini hasa walichokusanyikia akinadada hawa warembo. Katika picha hizo panaonekana palikuwa na sherehe ya nguvu na kukionekana maandishi yanayosomeka ‘Kisa’s Baby Shower’.

Udadisi wangu ukanipelekea kugoogle neno hilo na kujikuta kwenye blog ya William Malechela ambayo ilikuwa na picha nyingi na nzuri zaidi. Kwakuwa Google inajua kila kitu, nikaamua kutafuta maudhui ya sherehe hii ngeni kwangu lakini iliyopo miaka na miaka na miaka ili kuondokana na ushamba huu.Kitamaduni, sherehe za baby shower zilikuwa zikifanywa kwaajili ya mtoto wa kwanza wa familia na wanawake pekee ndio hualikwa kuhudhuria.

Madhumuni ya awali kabisa yalikuwa ni kuwapa wanawake fursa kubadilishana busara, masomo kuhusiana na ‘sanaa’ ya kuwa mama. Sasa hivi kimekuwa kitu cha kawaida kufanywa hata kwwa watoto wanaofuata ama wal wa kuasili yaani adoption.
Akina mama watarajiwa shereheni

Popping them bottles
Katika sherehe hizi zipo sheria kadhaa hasa katika kuchagua wapi na lini baby shower itafanyika.

Idadi ya waalikwa na aina ya burudani ama nguo za kuvaa huamliwa  mwenye sherehe, yaani yule anayetegemea kujifungua. Wengi hualika wanawake tu. Kama itafanyika baada ya mtoto kuzaliwa basi mtoto huletwa pia.

Zawadi kutokana na kazi za mikono
Hizi ni zawadi ambazo mtoto huja kupewa akizaliwa
Wageni huja na zawadi mbalimbali kumpa mama mtarajiwa. Zawadi hizi ni pamoja na nguo, nepi, chupa za maziwa ama midoli.

Maelezo hayo mafupi bila shaka yamekufumbua mwenzangu uliyekuwa na ushamba kama wangu kuhusu Baby Shower.

KABOTA
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!