Thursday, August 23, 2012

BAHATI BUKUKU ANUSURIKA KUPEWA TALAKA BAA

Bahati Bukuku.
STAA wa nyimbo za Injili Bongo anayetamba na albamu ya Dunia Haina Huruma, Bahati Bukuku amenusurika kulimwa talaka baa kutoka kwa mumewe waliyetengana naye miaka 7 iliyopita, Daniel Basila.

Kwa mujibu wa chanzo, ishu hiyo ilitokea mwishoni mwa mwezi Julai, mwaka huu ndani ya Baa ya Land Mark Hotel iliyopo Ubungo, jijini Dar.


Ilidaiwa kuwa, Basila alimwita ‘mtalaka’ wake huyo hotelini hapo ampe talaka yake baada ya kuishi ‘singo’ kwa miaka saba huku ndoa yao ikiwa haijulikani hatima yake.


“Daniel alimwita Bahati kwa simu, akamwambia aende pale hotelini akampe talaka. Alipofika alimkuta jamaa ameshika kikaratasi eti ndiyo talaka, lakini Bahati akamwambia kama amedhamiria kutoa talaka aende mahakamani,” kilisema chanzo
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!