Thursday, August 16, 2012

BELINA ALA SHAVU NONO....HIVI SASA NI BALOZI


Mwanamitindo Belina Mgeni.

MWANAMITINDO mwenye mvuto Bongo, Belina Mgeni amelamba shavu la nguvu kutoka kwa kampuni kubwa ya nywele nchini kwa kusainishwa mkataba wa mwaka mmoja kuwa balozi wa kampuni hiyo.


‘Akisemezana’ na waandishi wetu, Belina alisema anamshukuru  Mungu kwa kupata shavu hilo ambapo sasa picha zake zitakuwa zikionekana katika mabango ya kampuni hiyo, pia atakuwa akisuka bure nywele kwa kipindi cha mwaka mmoja na kutumia bidhaa za kampuni hiyo kama balozi.


Aidha, mwanamitindo huyo alisema ataubeba ubalozi huo kwa umakini mkubwa  kwa sababu heshima waliyompa ni kubwa sana  kwa upande wa warembo  na wanamitindo wa hapa nchini.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!