Monday, August 20, 2012

BOB LUDALA AITOSA INAFRICA BAND NA KUHAMIA KARUNDE BAND

Hivi karibuni hitmaker wa ‘Julie’ Bob Ludala aliitosa bendi yake ya Inafrica aliyokuwa nayo tangu mwaka 2001 na kuhamia kwenye bendi inayoongozwa na Deo Mwanambilimbi, Karunde Band.

Akiongea na kituo cha runinga cha TBC1 jumapili ya Eid Mosi, Bob Ludala alisema sababu zilizomfanya aondoke Inafrica ni kutokana na kuangalia sehemu atakayopata maisha zaidi.

Alisema mara nyingi bendi ya Inafrica imekuwa ikifanya show nyingi za nchi za nje lakini akagundua kuwa anajikuta yuko mbali kwa muda mrefu na akirudi nyumbani anakuwa hajafanya lolote na maisha yanaenda.

Na sasa akiwa Karunde Band amehusika katika utengenezaji wa albam mpya ya bendi hiyo iitwayo ‘Zimebaki Story’.

Katika hatua nyingine msanii huyo alisema wasanii wengi nchini wanaishi maisha magumu tofauti na watu wanavyowafikiria kwakuwa kazi zao hazinunuliwi kiuhalali.

Amewataka wananchi wawasupport wasanii kwa kununua kazi zao halali kama ilivyo nchi za nje na kuzipiga vita kazi haramu zinazouzwa mitaani.

Amewataka pia wasanii wa hapa nchini kuwa na utaratibu wa kusajili kazi zao COSOTA kwakuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wakiingiza pesa kutokana na matumizi mbalimbali ya kazi zao.

Alitolea mfano waliwahi kwenda nchini Australia ambako walijikuta wakishindwa kuperform baadhi ya nyimbo kama za Bob Marley kwakuwa walitakiwa kuzilipa kiwango ambacho wlaishindwa kukimudu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!