Monday, August 6, 2012

BOSI WANGU KAZINI ANANITAKA KIMAPENZI. YEYE NI MAMA MTU MZIMA NA ANA WATOTO. NAOMBA USHAURI WENU

Habari zenu, jamani mimi ni mara ya kwanza kuleta tatizo hapa, ni matumaini yangu nitafaidika na ushauri wenu. Mimi ni mwanaume nina miaka 26 , nafanya kazi kwenye kampuni moja hapa nchini.

Hivi karibuni hapa kazini kuna Mkuu  wangu wa kazi  ambaye  ni mama mtu  mzima  amekuwa akinitaka kimapenzi.Yeye ni  mke  wa mtu  na  ana watoto.Mume wake  hutumia muda  mwingi katika shughuli  za kibiashara nje ya nchi.

 Hivi karibuni amekuwa karibu sana na mimi.Ukifika muda wa chakula   huwaagiza wahudumu  wa cafe  waniletee  chakula ofisini eti  kwa sababu nipo busy na kazi.

Mara nyingi  huja ofisini kupiga stori na mimi,jambo linalonofanya nikose amani mbele ya wenzangu.

Kuna siku moja alikuja nilipokuwa nimekaa  ofisini kwangu  akaniwekea mkono begani halafu akaniangalia usoni kwa sekunde kadhaa karibu nianguke kwa uoga.Japo hajanitamkia ila nahisi ananitaka kimapenzi maana ni wazi kabisa.

Jumatano ya wiki iliyopita alinisubiri mpaka nikamaliza kazi,then  kanipa lifti mpaka maeneo fulani karibu na nyumbani kwangu.Wakati anaondoka akaniambia kuwa kuna safari ya  kiofisi itabidi niende naye  Mwanza   wiki  ijayo kwa ndege, kwa hiyo nijiandae.Yaani nime changanyikiwa  sana.

Ijumaa aliniachia ujumbe ofisini eti tukutane lunch. kufika kaniodea na chakula nikabaki nimeduwaa. 

Nilimuambia sitaweza kukaa kula maana nina kazi kibao ofisini nitabeba basi na yeye kabeba chake kaja kula ofisini kwangu alivyomaliza akakaa nikawa najaribu kupoteza lengo namuuliza mambo ya kazi lakini mara anishike mkono, mara aniangalie tu kwa muda usoni ili mradi tu ni kama mwanaume anavyomtongoza mwanamke vile.

 Sasa najiuliza nimuelezaje huyu mama kuwa mimi sipo tayari na sitaki kwenda  naye Mwanza . Mimi binafsi nina mchumba wangu ambaye tumetambulishana kwa  wazazi.Niliona kuwa  kabla  hatujafunga ndoa ni bora nitafute kazi ili maisha  yasitushinde.Bahati mbaya kazi inanitesa na kunipa mtihani mgumu

Nimechanganyikiwa   na sijui cha kufanya.Nikifikiria  nihame ofisi ,najiuliza  ntapata wapi tena kazi  na  elimu yenyewe yakuunga  unga.

Kilichonifanya nishtuke ni kadi aliyoninunulia siku chache zilizopita ,yaani ilikuwa ni ya kimapenzi kabisa . Wenzangu ofisini wameshaanza kuhisi vibaya.Nifanyaje  jamani.Naomba ushauri wenu  kupitia blog  yenu
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!