Sunday, August 5, 2012

CHADEMA Morogoro wakamatwa kwa kukaidi amri ya kutokufanya mkutano


Askari Polisi wa Kikosi cha Pikipiki ‘Chita’ na ambao hujulikana kwa jina jingine ‘Foda Fasta’ wameyakamata magari ya CHADEMA, yaliyokokuwa yakipita mitaani eneo la mzunguko wa Masika yakitangaza juu ya kufanyika kwa maandamano na mkutano wa hadhara Agosti 4, mwaka huu katika eneo la uwanja wa Shule ya Kiwanja cha Ndege Mjini hapa ambao ulipangwa kuhudhuriwa na Viongozi wakuu wa Chama hicho.

Magari hayo yalikamatwa na Mkuu wa Kituo Cha Wilaya cha Polisi wa Usalama Barabarani kutokana na kukaidi agizo la Polisi lakusitisha Mkutano huo.

Picha via blogu za Lukwangule na Juma Mtanda.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!