Thursday, August 23, 2012

FIESTA 2012 NDANI YA MOSHI MCHANA HUU

Sehemu ya Wanaharakati wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakiwa wamepozi mapema leo mchana mjini Moshi,mara baada ya kumaliza awamu yao ya kwanza ya kuruka hewani na amsha amsha ya tamasha hilo kwa wakazi wa mji wa Moshi,kutoka kulia pichani ni Bonge,Eric Kusaga,Simon Malenga sambamba na Millard Ayote wote kutoka Clouds FM.

Tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Moshi linatarajiwa kurindima ijumaa hii ndani ya Chuo cha Ushirika,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 5000 tu kwa kila mmoja,kama vile haitoshi kutakuwepo na wasanii lukuki wa bongofleva akiwemo na aliyeshiriki shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezzoo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!