Friday, August 31, 2012

GARDNER G HABASH ATUA RASMI TIMES FM


Mtangazaji na mjasiriamali Gardner G. Habash leo ametambulishwa rasmi katika kituo cha Radio Times FM na kumaliza uvumi uliokuwa umeanza kuenea wa wapi Gardner anaelekea, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili baada ya kujiuzuru kazi ya utangazaji katika msimu wa mwisho wa mwaka wa 2010.

Hafla ya kumtambulisha mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha Radio ya Clouds FM kwa waandishi wa habari itafanyika leo katika kiota cha chakula, vinywaji na burudani ya luninga za michezo City Sports Lounge ambapo Mtangzaji Scholastica Mazura  ndiye mhariri mkuu wa habari katika Radio Times Fm.

Gardner atakuwa akitangaza kipindi kinachoitwa Maskani ambacho kitakuwa kinaruka hewani kuanzia majira ya saa kumi alasiri mpaka saa moja usiku kuanzia siku ya Jumatatu ya Tarehe 3 Mwezi wa Tisa.

mpekuzi  inapenda kumpongeza bwana G Habash kuendeleza . Monalisa Na Mama yake ambao nao ni watangazaji wa kipindi cha Filominata kinachorushwa siku za jumapili Waandishi Wa Habari Wakipata Chakula Gardner akipozi pamoja na watangazaji wenzake wa Times FM Schola na Natasha Gradner akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Gardner akipozi na Kipi Malecela
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!