Sunday, August 26, 2012

GOLDIE AMTEMA PREZZO NA KUMFANYA ARUDI UGANDA BILA MAFANIKIO


Safari ya Prezzo nchini Nigeria imemrudisha bila kukipata kile alichokiendea baada ya Goldie kuonekana kutofurahishwa na ziara yake.


Prezzo aliyekuwa mshindi wa pili kwenye Big Brother Africa StarGame wiki hii alienda nchini Nigeria kuwaomba radhi wananchi wa huko na pia kutangaza nia ya kumfanya Goldie awe mke wake.

Katika mahojiano na waandishi wa habari jijini Lagos, Prezzo alisema alienda nchini humo kumuomba uchumba Goldie.
Hata hivyo hakufanikiwa kuonana Goldie ambaye Prezzo alisema hakuwa anapokea simu yake.

Hadi leo Goldie hajazungumzia chochote kuhusu ziara ya Prezzo.

Shabiki mmoja kupitia Twitter alimuuliza Goldie “Good afternoon madam, is it true that Prezzo is in town?” na yeye kumjibu “I also heard the pope is catholic. Is it true?”

Baadaye aliandika, “Gone R d days wen a problem shared is a problem solved; nowadays a problem shared becomes a topic of discussion. So keep ur problems 2urself!”

Kisha kuongeza: “Any1 can say anything, after all talk is cheap. But it’s in ur ACTIONS dat we’ll C ur tru intentions&where ur heart lies.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!