Wednesday, August 1, 2012

"Diamond Hatunae Tena" anasema ndiyo ingekuwa kichwa cha habari leo

Kwenye tovuti yake "www.thisisdiamond.com", Diamond anaandika:
Picture: Dkt. Hery Mwandolela na Diamond
Dkt. Hery Mwandolela akiweka "EKG/ECG leads" kwenye kifua cha Diamond
DIAMOND HATUNAE TENA...!!!

"Diamond hatunae tena"....hiyo ndo ingekuwa heading na kichwa cha habari cha media na watu wengi kwenye social networks na simu zao za mikononi kwa siku ya jana....

Kiukweli hali yangu ilikua ni mbaya sana, nilizidiwa na homa kali ya ghafla iliyosababishwa na kifua kilichonisumbua kwa takribani wiki mbili mfululizo.... hadi kupelekwa Heameda Medical Clinic kwa Doctor Hery M. Mwandolela, "Heart and Cough Specialist" kwa uchunguzi na vipimo vikubwa maana hali haikuwa ya kawaida..... namshkuru Mwenyezi Mungu baada ya vipimo vyote iligundulika ni kifua cha kawaida tu ila kilisababishwa na tour na ziara nyingi nilizozifanya mikoa na nchi mbalimbali kwa mfululizo bila mapumziko ya kutosha.

Kwa sasa hali yangu si mbaya sana... nawashukuru wote mliokuwa mkiniombea kupitia Blogs, Twitter, Bbm, Facebook...etc, na Media zote niweze recover.
Picture
Diamond
Picture
Picture
L-R: Dkt. Hery Mwandolela na Diamond
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!