Friday, August 3, 2012

HIKI NDICHO KIPYA ALICHOSEMA JAGUAR KUHUSU KUMSUPPORT PREZZO KWENYE BIG BROTHER.


Juzi Aug 1 2012 stori kubwa ya Jaguar kumdiss Prezzo kwenye page yake ya mtandao wa kijamii wa twitter kwamba Wakenya na Waafrika wengine wasimpigie kura kwa sababu hatakiwi kushinda hizo pesa za Big Brother ndio iliibuka.
Kila alieona hizo tweets alishtuka manake zilikua na maneno mazito na zilikua zinachana waziwazi.

Baada ya watu wengi kuamini kwamba ile account ni ya Jaguar, ameongea na kusema kwamba hana account ya twitter.

Amesema “nimeshtuka sana na nimepigiwa simu nyingi lakini sina account ya twitter, niko facebook tu na siku zote nimekua nikisema tumpigie kura Prezzo tumsupport kama Mkenya mwenzetu, namsupport kabisa kama kaka yangu kwa sababu zile hela hata zikienda kwa mtu mwingine labda Zambia au South Africa hazinisaidii, afadhali zichukuliwe na Mkenya mwenzangu”

Baada ya kuyasema hayo, Jaguar akamalizia kwa kutamka “tofauti zetu ni za muziki lakini sio yeye kwenda Big Brother, namsupport kwenda Big brother kwa sababu anahitaji hizo pesa sana sasa akizipata ndio aje tuonane, hata hivyo haitakua kitu kikubwa sana akishinda hizo milioni 24 japo itakua vizuri kwa sababu ndio tutaweza kukaa kama wanaume manake kipindi cha nyuma hatukuweza kwa sababu hakuwa na pesa, ndio maana namsupport sana sasa hivi ili nisikie ataongeaje akiwa na pesa kwa mfuko”

Jaguar na Prezzo bado wako kwenye beef ambayo ilianza longtime kidogo kwa Jaguar kusema kwamba Prezzo hawezi muziki na ishu zake za kujisifia mavazi na bling bling zimeshapitwa na wakati, pesa anazoringia ni za wazazi lakini yeye (Jaguar) pesa zake ni za jasho lake.
.
.
.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!