Wednesday, August 15, 2012

HUYU NDO MWANAMKE TAJIRI NA MREMBO KULIKO WOTE UGANDA

JARIDA  maarufu la  Times nchini  Uganda  limemtaja mama wa watoto wawili Zari Hassan kuwa ndiye mwanamke mrembo na tajiri kuliko wote nchini humo kwa wakati huu.

Kwa  mujibu wa  jarida hilo Zari (30) ambaye ni Mwanamuziki,Mfanyabiashara na Mtangazaji wa  runinga  amepata mafanikio makubwa  kwenye  muziki na pia  kipindi chake cha runinga  kinachofananishwa na  kipindi cha ‘Keeping up with the Kardashians’ kinachoendeshwa na mrimbwende wa kimarekani Kim Kardashian.

Huku likiambatanisha picha za magari na  nyumba  anazomiliki mwanadada huyo, jarida hilo limeandika  kuwa  huenda akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika baada ya kipindi kifupi kijacho endapo ataendelea na mwenendo wake wa sasa kibiashara.

hata  hivyo jarida hilo pia  limetaja  zari kuwa mmoja wa mstaa wapenda starehe na  amekuwa  akitumia  mkwanja alionao kumnasa  mwanaume wa aina yoyote anahisi kuwa  anahitaji kumliza kwa wakati huo ingwa tuhuma hizo hazikusibitishwa moja kwa moja.

katika  hatua nyingine jarida hilo limesema  kuwa Zari mwenye maskani yake pia  nchini Afrika ya Kusini, wazazi wake si raia wa uganda kuzaliwa ispokuwa ni wahamiji kwani baba  yake ni raia wa Burundi mwenye asili ya Somalia na mama yake ni raia wa India kutoka  kabila la Mutoroo.

Aidha Times limeandika  kuwa Zari anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama  BMW – 2006, Black Chrysler – 2008,  – Audi Q7 2010 Silver Crysler – 2008, JETTA-2006, Mercedes Benz convertible -2008. Range-Rover, Lamborghin, Hummer na  mengine mengi huku pia  akiwanaumiliki wa maduka, hotel na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria, Cape Town na Kampala.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!