Thursday, August 2, 2012

IKULU:Rais Jakaya Kikwete Amteua Bi Karolina Albert Mthapula kuwa Msaidizi wa Rais – Kitengo cha Uchumi (Masuala ya Elimu).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi Karolina Albert Mthapula kuwa Msaidizi wa Rais – Kitengo cha Uchumi (Masuala ya Elimu).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Agosti Mosi, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, inasema kuwa uteuzi huo unaanza leo hii.

Kabla ya kuteuliwa kwake, Bibi Mthapula alikuwa Ofisa Elimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Agosti, 2012
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!