Wednesday, August 22, 2012

" IMANI ZA KISHIRIKINA" ZAMFANYA MAINDA AKATALIWE UKWENI ( MAMA RAY )

Mwigizaji wa picha za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ anadaiwa kukataliwa ukweni na mkwewe wa kike anayefahamika kwa jina la Mama Kigosi au Mama Ray.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, mama Ray hampendi Mainda kiasi cha kutopenda kumuona akifika nyumbani kwake.

 “Unajua mama Ray hampendi Mainda, aliwahi kumwambia Ray kuwa, asimuone msichana huyo nyumbani kwake kwani anahisi yeye ndiye anayumbisha maisha ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuipata habari  hii ,waandishi wetu walimtafuta  Mainda  ambaye  alikuwa  na haya:

"Jamani, jamani hivi ni nani kasema?, kwanza mimi sijawahi kwenda kwa mganga hata siku moja, nimeokoka na siwezi kufanya hivyo.

“Ninajua wanaoleta habari hizo ni Bongo Movies, sijui nimewakosea nini . Ray  ananipenda   mwenyewe  na sijawahi  tumia  dawa"
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!