Saturday, August 18, 2012

‘IRENE UWOYA’ AJIPANGA YA KUFANYA KAZI NA NYOTA WA NIGERIA NA GHANA…!!


WAKATI filamu nyingi za Tanzania zikiwa zinafanya vizuri kwenye masoko makubwa ya filamu ya nchini Ghana na Nigeria na Afrika kwa ujumla, msanii Irene Uwoya amedai kuwa kabla ya kumalizika kwa mwaka huu atafanya mchakato wa kutengeneza filamu na wasanii kadhaa wa nchini hizo ingawa bado anajipanga kwenye suala zima la fedha.
Akiongea na Mwandishi  wetu 
,Uwoya alidai kuwa amekuwa akiweka ukaribu na kujenga urafiki na baadhi ya nyota wa filamu wa nchi hizo ili hata pale atakapoamua kuwashirikisha kwenye filamu zake iwe rahisi.

“Ni kweli tunahitaji kudumisha ukaribu kati ya Tanzania na nchi hizi mbili ambazo zinafanya filamu zinazoendana na sisi hivyo kwa upande wangu kama msanii ninayefanya vizuri nina hamu ya kucheza filamu moja na nyota wa nchi hizo, hivyo kwa sasa naweza kusema najipanga kwa hilo,”
alidai.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!