Friday, August 24, 2012

JACKLINE WOLPER AMEANZA KUTENGENEZA FILAMU ZAKE MWENYEWE.....HUU NI MWANZO MZURI


Baada ya muigizaji mkongwe Hashim Kambi kuanza kutayarisha filamu zake mwenyewe, Jackline Wolper naye ameunga tela.

Muigizaji huyo mrembo amesema kupitia kampuni ya JB Production, ataanza kuandaa filamu zake.


Katika azma hiyo, Wolper atasaidiwa na meneja wake Leah Mwendamseke aka Lamata.


Vyanzo vimedai kuwa tayari kampuni hiyo imekamilisha kurekodi filamu iitwayo Malipo ni Hatari.


“Nimeingia katika fani ya utayarishaji na kwa kuanza ninakuja na filamu ya Malipo, ni filamu ya kipekee kuanzia hadithi, waigizaji wake wameigiza katika kiwango kikubwa cha kimataifa , okay sisemi mengi bali mtaona katika filamu ya Malipo,” Jack aliuambia mtandao wa FC.


Miongoni mwa waigizaji walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na yeye mwenyewe, Blandina Chagula ‘Johari’, Stanley Msungu ‘Seneta’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Mgata, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo, Slim na wengine.


Malipo ni Hatari imeongozwa na Lamata.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!