Friday, August 17, 2012

JIBU ALILOTOA WAZIRI MKUU BAADA YA KUULIZWA KUHUSU GAZETI LA MWANAHALISI.
Kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA alisimama na kumuuliza Waziri mkuu.

Namkariri akiuliza “sheria tunayoizungumzia iiyotumika kulihukumu gazeti la Mwanahalisi ni sheria ambayo imelalamikiwa na wadau wengi wa vyombo vya habari kwa muda mrefu  na ni sheria ambayo inaipa Serikali mamlaka ya ziada kuyadhibiti au bila hata kuyasilikiliza au kuvisikiliza vyombo vya habari pale vinapokua pengine vimeandika taarifa ambazo hazitaipendeza Serikali.


Madam sheria hii ya msingi ndio imekua tatizo kubwa, wewe huamini Muheshimiwa Waziri mkuu kwamba kutumia sheria mbaya ama sheria kandamizi kunyima haki ni msisitizo wa utawala usio bora?
.
Alichojibu Waziri mkuu ni hiki….. “mimi siamini hivyo muheshimiwa Spika kwa sababu sheria ile imetungwa na bunge lako hili tukufu kwa hiyo ilimradi bado ipo inatumika, ni sheria halali, yaliyomo humo ndio mliosema yako halali kwa hiyo sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapokua imerekebishwa”
 
Mbali na hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali haitoogopa vikwazo vyovyote vitakavyowekwa na nchi wahisani kufuatia kuzisimamisha meli zinazotuhumiwa kupeperusha bendera ya Tanzania wakati asili yake ni Iran.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!