Wednesday, August 8, 2012

JIHADHARI NA KANSA YA INI- SEHEMU YA PILI

 
Ugonjwa wa cirrhosis ni nini?

Cirrhosis ni matokeo ya ugonjwa sugu wa ini ambao  hubadilisha tishu za kawaida za ini kwa njia ya fibrosis, scar tishu, matezi (regenerative nodules),  kuziba damu kuingia kwenye ini  na hivyo kufanya ini kushindwa  kufanya kazi yake vizuri.


Visababishi vya ugonjwa huu

Cirhosis husababishwa na mjumuiko wa magonjwa mengi ambayo ni;


  1. Ugonjwa wa ini unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu ( alcoholic liver disease) .
Ugonjwa huu wa ini unaotokana na unywaji pombe kwa muda mrefu (alcoholic liver disease) hauathiri wanywaji pombe wote na si lazima uwe mnywaji pombe ili upate ugonjwa huu.
 
Wanywaji pombe kupindukia pia wanaweza kupata tatizo la utapia mlo (malnutrition) kutokana na pombe kukosa virutubisho muhimu vinavyohitajika  mwilini, kupungua kwa hamu ya kula, na kupungua kwa ufyonzwaji wa virutubisho  vya chakula  kwenye utumbo. Utapia mlo pia husababisha ugonjwa wa ini.

 
Alcoholic hepatitis ni hatari sana kwani unaweza kusababisha kifo.
 
MAMBO MENGINE YANAYOSABABISHA KANSA YA INI
  1. Non alcoholic steatohepatitis (NASH)  ama Non alcoholic liver cirrhosis   – Mafuta hujikusanya kwa wingi kwenye ini na kusababisha huharibifu wa tishu za ini (scar tishu). Ugonjwa huu unahusishwa na kisukari, unene uliopitiliza, utapia mlo wa protini (protein malnutrition), baadhi ya magonjwa ya moyo na baadhi ya madawa aina ya corticosteroids. Mgonjwa hapa hana historia ya unywaji pombe.
  2. Ugonjwa aina ya hepatitis B, C, na D, ambayo husababishwa na virusi vya hepatitis. Hepatitis B ndio chanzo kikuu cha ugonjwa wa cirhosis kati ya hepatitis zote duniani. Hepatitis C ndio sababu kuu ya wagonjwa wengi kuhitaji ini la kupandikizwa (liver transplant) duniani.
  3. Autoimmune hepatitis – Husababishwa na mfumo wa kinga mwilini ambao huathiri ini na kuharibu chembechembe au seli za ini na hivyo kusababisha ugonjwa wa cirrhosis.
  4. Magonjwa ya kurithi kama cystic fibrosis, wilson’s  disease, galactosemia, alpha 1 antitrypsin deficiency, hemochromatosis na glycogen storage disease. Watu wenye tatizo la ukosaji wa alpha  - 1  -antitrypsin  ambayo inakuwa kwenye mapafu ya binadamu na husaidia kukinga tishu zisiharibiwe na enzyme za seli za uhabirifu hasa nuetrophil elastase, wanaweza kupata mjumuiko wa magonjwa yanayoathiri mfumo wa upumuaji  (COPD)  kama watakuwa na historia ya uvutaji sigara.
  5. Cardiac  cirrhosis  - Hutokana na ugonjwa sugu wa moyo unaoathiri  sehemu ya kulia ya moyo na hivyo kuufanya moyo kushindwa kufanya kazi yake vizuri na hatimaye kulileletea madhara ini. Husababishwa na tatizo kwenye kizibo cha moyo (valve problem), kuathiriwa kwa moyo na maradhi ya bakteria au virusi, uvutaji sigara na nk.
  6. Madawa na sumu  zinazoharibu na kudhuru ini
  7. Ugonjwa wa kichocho (schistosomiasis)
  8. Magonjwa yanayojulikana kama  primary biliary cirrhosis na primary  sclerosing  cholangitis. 
  9. Makala ijayo tutaangalia dalili na viashiria vya cirrhosis.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!