Tuesday, August 7, 2012

JIHADHARI NA KANSA YA INI- SEHEMU YA KWANZA

 

JAMANI  KANSA  YA INI SIKU HIZI INAUA SANA. TUMEAMUA  KUANDAA  SOMO  KAMILI JUU  YA  GONJWA  HILI HATARI. 

 SOMO  HILI  LIMEGAWANYIKA SEHEMU TANO.KILA SIKU TUTAZUNGUMZIA  SEHEMU MOJA.KARIBUNI.

 Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu. Ndicho kiungo kikubwa kilichopo ndani ya mwili. 

Ugonjwa wa cirrhosis ni ugonjwa wa 12 duniani kati ya magonjwa yanayosababisha vifo vitokanavyo na  maradhi.

Cirrhosis husababishwa na unywaji pombe kupindukia, ugonjwa wa hepatitis B, C, na ugonjwa wa fatty liver disease. 

Kabla ya kuangalia ugonjwa wa cirhosis  (tamka sirosis kwa kiswahili), kwanza tuangalie kazi ya ini kwenye mwili wa binadamu.

Ini linahusika na;


 • Kushughulikia chakula kilichosagwa kutoka kwenye utumbo mdogo (small intestine)
 • Hulinda mwili dhidhi ya magonjwa
 • Kutengeneza  nyongo (bile)
 • Hudhibiti kiwango cha mafuta, sukari na chembechembe zijulikanazo kama amino acids kwenye damu
 • Huhifadhi vitamini, madini ya chuma na kemikali nyengine muhimu
 • Huvunjavunja chakula na kutengeneza energy inayohitajika mwilini
 • Ini hutengeneza chembechembe zinazozuia damu kuganda mwilini kama fibrinogen, prothrombin, factor V, VII, IX, X  na X, protini C na S, antithrombin na nk.
 • Huharibu sumu na madawa ambayo yameingia mwilini.
 • Hutengeneza homoni aina ya angiotensinogen  ambayo inahusika kupandisha presha ya damu mwilini wakati inapokutana na enzyme ya renin, enzyme hii ya renin hutolewa na figo wakati figo inapohisi presha imeshuka mwilini.
 • Husafisha damu kutokana na chembechembe  mbaya na bakteria.
 • Hutengeneza enzyme na protini ambazo zinahitajika mwilini kwenye shughuli nyingi na hata kurekebisha tishu zilizoharibika. 
 • >>>makala ijayo tutaangazia ugonjwa wa cirrhosis ni nini?
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!