Wednesday, August 8, 2012

JITAHIDI KUMRIDHISHA MPENZI WAKO MNAPOKUWA FARAGHA

Mapenzi ni wote wawili kufurahia...hayo ndiyo mapenzi! Yaani unapokuwa na mpenzi wako kwenye uwanja wa sita kwa sita, wote mnatakiwa kupata kile kitu kinachotakiwa.

Lakini kumekuwa na malalamiko ya upande mmoja kumlaumu mwenzake kuwa hamtoshelezi sana, au mwingine anaonekana kujifikiria zaidi yeye kuliko mwenzake. Hilo ni tatizo kubwa sana kwa wapenzi.

Inawezekana kabisa wewe upo katika uhusiano na mpenzi wako kwa muda mrefu sana, lakini hata siku moja hujawahi kufurahia mapenzi. Pia si ajabu kwamba, hujawahi kufika kileleni tangu siku ulionza kuwa katika uhusiano na mpenzi wako.

Lakini pia, upo mjadala kwamba, ni nani kati ya mwanamke na mwanaume huwa haridhiki zaidi kimapenzi kuliko mwenzake? 

Kwa heshima kubwa, naomba kuuwasilisha kwenu, nikitaka maoni yenu, ukieleza kwa ujuavyo wewe kati ya mwanaume au mwanamke ni nani anawahi kufika mshindo na kumuacha mwenzake bado ana kiu?

Je, wewe ni jinsia gani? Unaridhishwa na mapenzi ya mpenzi wako? Kama ndivyo kivipi? Kama siyo, kwanini? Si vibaya pia kama utaeleza nini kifanyike, ili wapenzi wanapokuwa faragha, wapate usawa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!