Tuesday, August 14, 2012

JOAN: NINA SIFA ZOTE ZA KULITEKA SOKO LA FILAMU HAPA NCHINI


MWIGIZAJI Chipukizi katika tasnia ya filamu Joan Philipo amejigamba kwa kusema kuwa pamoja na kuwa msanii chipukizi anaamini kuwa ataliteka soko la filamu na tasnia kwa ujumla kwa sababu amejipanga kufanya kazi tena kwa nguvu moja.

Akiongea na mpekuzi alisema kuwa ameingia katika tasnia ya filamu huku akijua kuna upinzani katika fani hiyo.“Ninaamini kuwa haya ndio maisha yangu na ili niweze kudumu katika tasnia ya filamu ni lazima niwe makini.

Najua kila mtu kwa sasa anatamani kuigiza na kuwa nyota, kwa kuandikwa sana katika vyombo vya habari lakini kwangu si hivyo niandikwe kwa ajili ya kazi, nia yangu nikuwapoteza wakongwe wote waliopo katika sanaa,”anasema Joan.

Msanii huyo mwenye umri mdogo anajivunia kuwa ni mmoja kati ya wasanii waliotolewa na mwingizaji na muongozaji wa filamu wa  hapa nchini, Rose Ndauka.

Joan anasema kuwa alipata urahisi wa kuigiza kwa sababu filamu yake ya kwanza kuigiza aliongozwa na mwanamke ambaye ndiye Rose Ndauka anaamini kuwa hiyo ilimpa moyo wa kujiamini.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!