Monday, August 13, 2012

JOSE CHAMELEONE AANZISHA KUNDI LA MAENDELEO LIITWALO MOTO MOTOMwanamuziki wa Uganda  Jose Chameleone ameanzisha kundi la shughuli za maendeleo liitwalo Moto Moto.

Amesema kundi hilo halitajihusisha na siasa bali kufanya kazi ya kuwahimiza wananchi wa Uganda kufanya kazi na kuchangia shughuli za maendeleo pamoja na kuachana na tabia ya kufanyiwa kila kitu na serikali.

Amesema ameshaachia wimbo wenye jina hilo ili kusaidia kupigia debe shughuli za kundi hilo.

“Maisha yetu yapo mikononi mwetu, naishi kwenye nchi hii na naona kinachotokea mbele yangu. Mimi sio kipofu wa kushindwa kuona ongezeko la bei ya mafuta ya kupikia, sukari, ada za shule na vingine.

  Naona watu wakihitimu Makerere na shahada bila kazi, nasikia watu wakilalamika kuhusu serikali na wabunge hawafanyi kwaajili yetu, lakini tunahitaji kuacha kulalamika na kutafuta mabadiliko tuyatakayo", aliuambia mtandao mmoja wa Uganda.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!