Thursday, August 23, 2012

JUMUIA YA UAMSHO NI WACHONGANISHI NA WANALENGO BAYA KWA TAIFA HILI. SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKEMATUKO  HAYA   YANAFANYWA  NA KUNDI   LA UAMSHO   HUKU  WAKITAKA   KUJIFICHA  KUPITIA   TAASISI  ZA KIDINI.
TAASISI  HIZO  LEO  ZIMEKANUSHA  VIKALI  KUHUSIANA  NA MADAI   YA KUPINGA SENSA YA   WATU  NA  MAKAZI........
HAYA   NDO  MAELEZO  YAO 

*********************************************************

Taasisi mbalimbali za kidini hapa nchini zilizopata usajili rasmi kwa Mrajis Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekanusha kuhusika na tamko lililotolewa na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mselem Ali la Waislamu wa Zanzibar wagomee kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi Kitaifa inayotarajiwa kufanyika  Jumapili ijayo.

Wakizungumza na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga Wawakilishi wa Taasisi hizo wamelaani tabia ya Uamsho ya kujipa Mamlaka ya kuzisemea Taasisi hizo.

Aidha,wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuthibitisha ni kikao gani kilichokaa na kuzungumza na Taasisi za Kidini na kuamua kwa pamoja kutowa tamko hilo la kupinga kushiriki kwa Waislamu katika Sensa.

Aidha, wameihakikishia Afisi ya Mufti na Serikali kuwa watashiriki katika Sensa ili kusaidia maendeleo ya Zanzibar na kutatua baadhi ya migogoro ya kijamii na sio kujiingiza katika siasa na kupingana na Serikali kama ambavyo imekuwa ikifanya Jumuiya ya Uamsho.

Taasisi zimewataka Waislamu kushirikiana na Serikali na kuachana upotoshaji unaofanywa na Uamsho.

Aidha, wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuachana mara moja kutumia kivuli cha umoja wa Taasisi za kidini Zanzibar wanapoamua mambo yao kwani Jumuiya hizo nyingi hazikubaliani na Sera yao ya fujo na vurugu.

Mwisho.
 Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzibar
23/08/2012==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!