Monday, August 6, 2012

KAKA YETU NI SHOGA.....TUMEJARIBU KILA MBINU ZA KUMBADILISHA LAKINI TUMESHINDWA. TUNAOMBA USHAURI WENUNatumaini mu wazima. leo ninajambo moja zito sana na kwakweli nahitaji msaada wenu, kwetu tumezaliwa wanne wasichana watatu na mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 27 ambaye kwa kushangaza amekuwa shoga.

ilianza kama utani kwani hatujawahi hata siku moja kumuona akileta mwanamke nyumbani kwamba ni girlfriend wake ila mara kwa mara alikuwa anakuja na kundi la wanawake ambao ni mashoga zake kwa wakati huo sisi hatukugundua kitu kabisa.

lakini kwa muda tukawa tunamgundua anajipenda sana kupita kawaida, akawa anatembea na kibegi ambacho kutwa hakikosi manukato, lotion, kitana na mafuta ya mdomo kidogo, kwakweli tulishtushwa sana tukajuwa labda ni cha marafiki zake lakini mara kwa mara akawa nacho na pindi tukiamua kutoka pamoja kila mara huchukuwa kioo chake kidogo na kujiremba ndipo tulipojuwa kuwa ni bwabwa.

kwa kweli hiki kilitushtua sana na kwa vile wazazi wetu hawapo tena hatukuwa na mtu wa kuongea naye tukajitahidi kuongea na huyu kaka tukimshawishi aache ushoga lakini akatuambia anaupenda na hawezi kuuacha na tukiendelea kumshawishi atakimbia nyumba na asirudi tena.

kinachonikasirisha ni pale ninapomsikia akiongea na simu na hao wanaume wake anavyowaambia jinsi walivyomchanganya kwa mapezi jana yake na jinsi alivyokuwa anatamani tena, na wakati mwengine yupo busy kutuma message zake mbaya ambazo hazina adabu kabisa.

tunampenda sana huyu kaka yetu na hatutaki awe shoga tumejaribu kila njia ya kumwachisha lakini tumeshindwa jamani tusaidieni japo hata kwa mawazo tumfanyaje?

JOYCE.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!