Thursday, August 23, 2012

KAMA KAWAIDA: BIG BROTHER AFRICA YAMPA "MCHUMBA" PREZZO AMBAYE AMELAZIMIKA KUOMBA MSAMAHA HADHARANI


Mshindi wa pili wa Big Brother Africa Stargame Jackson Makini aka Prezzo yupo nchini Nigeria ambako ameenda kuwaomba radhi wananchi wa nchi hiyo.

Habari njema kwa mashabiki wake ni kuwa jamaa ana mpango wa kumuoa Goldie kama akilikubali ombi lake.
Rapper huyo mwenye miaka 32 amesema hajasafiri kutoka Kenya hadi Nigeria ili kucheza tu bali kwenda kuelezea hisia zake kwa mwanamke ambaye Mungu aliwakutanisha naye kwenye jumba la BBA.

Katika mahojiano na waandishi wa habari nchini Nigeria, Prezzo, amewaomba radhi wanaijeria kwa namna alivyomfanyia Goldie mjengoni humo na kutangaza hadharani kuwa yupo tayari kufanya lolote ili amfanye Goldie mkewe.

‘I was not able to express all my feelings to Goldie in the house due to paranoia and I am ready to come and fight for a prize that worth it and that will make me a real winner…’ alisema Prezzo.

Tatizo ni moja. Goldie hapokei simu yake. Is it too late too little?

BOFYA KITUFE   CHA "PLAY"   ILI  UMSIKILIZE==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!