Sunday, August 26, 2012

KANYE WEST AJARIBU KUWASULUHISHA D'BANJ NA DON JAZZY


Katika jitihada za kurudisha urafiki na producer wake wa zamani,  mwanamuziki wa Nigeria , D’Banj anadaiwa kumuomba rapper Kanye azungumze na Don Jazzy.


Kwa mujibu wa ripoti, mmiliki huyo wa DB Records anafanya kila awezalo ili aumalize ugomvi alionao na mmiliki mwenzie wa iliyokuwa Mo’ Hits Records, Don Jazzy.

Miezi michache iliyopita Kanye alimpigia simu Don Jazzy kujaribu kuwaomba nguli hao wasahau yaliyopita na kufanya kazi tena.

Chanzo kimoja kilicho karibu na D’Banj na Don Jazzy kimethibitisha kuwa ni kweli D’Banj amekuwa akijaribu kumrudisha Don Jazzy na amefanya hivyo kwa muda sasa.

“Kanye West, anaaminika kuwa katikati ya mgongano huo uliosababisha wagombane na anajaribu kuwasuluhisha.  Kanye West hakuwa anajua kuwa kuna ugomvi kati ya D’Banj na Don Jazzy mpaka miezi mitatu iliyopita na amekuwa akijaribu kuwarudisha pamoja,” kilisema chanzo hicho.

Inadaiwa kuwa alipokuwa studio na D’Banj wiki kadhaa zilizopita wakati wakifanya remix ya Scapegoat, Kanye West aliianzisha mada hiyo tena na kumuuliza D’banj kwanini Don Jazzy hakuwepo naye  Marekani kufanya wimbo huo pia. D’Banj anadaiwa kumwambia kuwa bado ni marafiki lakini wanafanya kazi tofauti sasa.

Ripoti hizo zimedai kuwa D’Banj alimwalika Kanye West kwenda Nigeria kwaajili ya kufanya naye video ya remix ya Scape Goat. Kanye alikubali lakini kwa masharti kuwa atakuja baada ya D’Banj kuyamaliza na Don Jazzy na yeye awepo kwenye video hiyo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!