Thursday, August 16, 2012

KOLETA AWALAUMU WASANII WA BONGO MOVIE KWA KUTOMJULIA HALI....

 

MWIGIZAJI wa longtime katika tasnia ya filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ juzikati ameibuka na kusema hajawaelewa baadhi ya wasanii wa Bongo Movie Club kwa kutokwenda kumjulia hali alipolazwa kwa siku tano katika Hospitali ya Kairuki, Dar akisumbuliwa na Kidole Tumbo ‘Appendix’ wakati kila siku wanahubiriana upendo miongoni mwao.

“Sijawaelewa kabisa Bongo Movie, mimi ni mwanachama, huwa nashirikiana nao vizuri wakati wa matatizo lakini yamenifika mimi eti wanadai wako ‘location’, wengine kambini, wale waliokuwa nje ya mkoa siwalaumu.”

Kwa upande mwingine, Koleta aliwashukuru wale waliokuwa bega kwa bega na yeye katika kipindi hicho wakiwemo wasanii wa Kundi la Kaole, wasanii wa Bongo Movie Club ambao ni Batuli, Devotha Mbaga, Herieth Chumila, Chiki Mchoma na Jacqueline Wolper.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!