Monday, August 13, 2012

KUMBE NYWELE ZA NAOMI CAMPBELL NI FEKI....


BAADA ya kuonekana mrembo kwa miaka mingi, mwanamitindo mkongwe Naomi Campbell, wiki iliyopita aliwashangaza wengi baada ya kubainika kuwa sehemu kubwa ya nywele zake kichwani hasa sehemu ya mbele zimenyonyoka na anastiliwa zaidi na nywele za bandia.

Picha za muonekano wa modo huyo mwenye umri wa miaka 42 zilinaswa wiki iliyopita alipokuwa amemaliza kuogelea katika pwani ya Ibiza.


Mara baada ya kutoka kwenye maji, muonekano wa kichwa chake kilicho ulionekana vizuri kwa kuwa nywele zilikuwa zimelowa maji. 


Kwa miaka mingi Naomi amekuwa akionekana na nywele za bandia, hivyo kitendo cha kuonekana hivyo kiliwashangaza wengi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!