Wednesday, August 8, 2012

KUTOKA SHINYANGA: MAMIA WASHIRIKI MBIO ZA BAISKELI ZA SAFARI LAGER KANDA YA ZIWA

 Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Safari Baiskeli Kanda ya Ziwa, wakijiandaa kuondoka kwenda Kahama na kurudi katika Uwanja wa Kambarage ikiwa ni maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane inayoadhimishwa leo nchini kote
Baadhi ya washiriki wa mbio za Safari Baiskeli Kanda ya Ziwa, wakiwa maeneo ya Kagongwa wakielekea Kahama wakati wa mashindano hayo yaliyoenda sambamba na maadhimisho ya Sikukuu ya Nane Nane yanayofanyika leo nchini kote.

Washiriki wa Mashindano hayo waliendelea kuchanja mbuga kuelekea Kahama na baadae kurejea Shinyanga mjini.
Waendesha baiskeli wanawake ambao nao hawakuwa nyuma katika kushiriki mbio hizo waki tayari kwa safari ya kwenda Kahama na kurudi Shinyanga mjini kwa baiskeli.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!