Saturday, August 18, 2012

LADY JAYDEE AMPIGA VIJEMBE ANETH KUSHABA WA SKYLIGHT BAND

Katika kile kinachoonekana kuwa Lady Jaydee ameanza kuogopa moto wa bendi mpya ya SkyLight inayoongozwa na Aneth Kushaba, kiongozi huyo wa bendi ya Machozi ameitupia madongo bendi hiyo.

“Its not about making noise na mabango. Debe likiwa tupu ni tupu tu. Its all about what u can do,” ametweet Jaydee mchana wa Jumamosi.

Tweet hiyo iko wazi kwakuwa anazungumzia mabango yanayoonekana kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yakiwa yamebebwa na akinadada waliolipwa kufanya kazi hiyo.


Hivi karibuni aliyekuwa muimbaji wa bendi ya Machozi, Sam Machozi alihamia kwenye bendi hiyo inayokuja juu nchini ambayo Eid mosi na Pili itapiga show Girrafe Ocean View  Hotel.

Je hii ni ishara kuwa Jaydee anauhofia ujio wa SkyLight band?
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!