Wednesday, August 8, 2012

“LINAH” AONGELEA UJIO WA NGOMA MPYA, GARI YAKE AINA YA BMW NA UPCOMING UK TRIP…!!MSANII anayefanya vizuri kwenye soko la muziki wa kizazi kipya kwa upande wa wanawake Linah Sanga ‘Linah’, a.k.a Ndege Mnana ameumbia mtandao wa mpekuzi kuwa baada ya kutoka Marekani alikoenda kikazi sasa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ushafahamu’, ambayo itaigia sokoni siku chache zinazokuja.

Akilonga na mwandishi wa 
mpekuzi, Linah, alisema kuwa ngoma hiyo itakuwa ni ya kwanza kutoa tangu aliporudi kutoka nje hivyo anaamini itafanya vizuri kwani maandalizi na uwezo wake katika kazi hiyo ni mkubwa mno.Linah akiwa na mashabiki wake kwenye moja ya show alizofanya USA


Alisema kuwa ikiwa sokoni ngoma hiyo atakuwa katika mchakato wa video , ili mashabiki wake wapate burudani zaidi kutoka kwake.


“Hiyo ni ngoma ambayo nimeifanya mwenyewe baada ya kutoka Marekani, lakini ipo nyingine pia ambayo nimefanya na Amini, ambayo hata hivyo jina la ngoma hiyo nahisi itaitwa ‘Linah na Amini’, kwa sababu tumefanya si tu kwa kushirikishishana bali kwa ushirikiano,”
alisema.

Hata hivyo mwadada Linah aliongeza kuwa anatarajia kusafiri kikazi kwenda
UK ambapo atakuwa huko kanzia Agosti 23-24.

Sambamba na michakato hiyo hakusita kueleza kuwa katika kujiimalisha kimaisha tayari amesha nunua mkoko mpya aina ya
BMW
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!