Saturday, September 1, 2012

LINAH KUPIGA SHOW YA NGUVU NCHINI UINGEREZA LEONchi za nje kwa sasa wanamuita ‘The Queen of Bongo Flava’!! Vipi kuhusu Lady Jaydee na Ray C? Huenda watanzania waishio nchi za nje wameamua wenyewe kumpa crown ya umalikia wa muziki wa Bongo mrembo huyu wa THT. Kwa mara ya kwanza kesho, Linah Sanga atapiga show nchini Uingereza.Watanzania na wapenzi wengine wa muziki waishio Uingereza watakuwa wananchi wa nje ya Tanzania wa kwanza kuusikia live wimbo wake mpya uliotoka siku za hivi karibuni, Ushafahamu Nakupenda.

Miezi miwili iliyopita Linah aliyetamba na ngoma kama Fitina na Angalau alikuwa na ziara ndefu ya nchini Marekani ambako alikaa kwa karibu miezi mitatu.Huo ni mwanzo mwingine mzuri wa mashavu zaidi ya show za nje kwa mwanadada huyo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!