Friday, August 3, 2012

Mahakama ya EAC yatangaza kufungua masijala ndogo nchi za Rwanda,Burundi,Kenya,Uganda na Tanzania leo.

 Msajili wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,Dk John Ruhangisa akifafanua jambo wakati akitangaza mpango wa mahakama hiyo kufungua masijala ndogo katika nchi za Rwanda,Burundi,Kenya,Uganda na Tanzania leo

  ======  ========  =======
Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EACJ)imeanzisha Masijala  ndogokatika nchi wanachama ili kuwawezesha wananchi na taasisi zenye lengo la kufungua kesi kwenye mahakama hiyo kufanya hivyo katika nchi zao.

Msajili wa Mahakama hiyo,Dk John Ruhangisa amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu sana na ambayo imekuwa ikisubiliwa kwa hamu na wananchi ambao wamekuwa hawawezi  kufika yalipo makao makuu ya mahakama hiyo mjini Arusha.

Amesema  uzinduzi wa Masijala ndogo ya kwanza ya EACJ utafanyika Kigali nchini Rwanda wakati wa utoaji tuzo kwa waandishi bora wa habari zinazohusu jumuiya hiyo.Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni  Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi. Mbali na hilo pia Mahakama hiyo iko mbioni kusajili kesi kwa njia ya mtandao kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kukua kila siku na mahakama hiyo kuona ukuhimu wa kwenda na wakati
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!