Saturday, August 4, 2012

Malawi yakataa tamko laTanzania kuhusu gesi

Malawi imekataa kuitikia wito uliotolewa na serikali ya Tanzania  wa kuitaka isimamishe shughuli za kutafuta mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa, wakati suluhu ya mvutano wa mpaka ikisubiriwa. 

Vita vya maneno vimezuka kati ya nchi hizo mbili baada ya Malawi kuipa leseni Kampuni ya Uingereza kufanya utafiti katika eneo hilo. Maafisa nchini Tanzania wanasema  kwamba, mvutano huo uliodumu kwa miaka 50 sasa unaweza kuwa mkubwa iwapo ugunduzi wa mafuta na gesi utatokea kwenye ziwa hilo linalojulikana pia kwa jina la Ziwa Malawi. 

Serikali ya Tanzania inasema inaendelea kufanya mazungumzo na Malawi na iko tayari kuwasilisha suala hilo kwenye vyombo vya upatanishi. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Bernard Membe amesema, suala hilo ni nyeti sana na Tanzania ingependa litatuliwe kwa maelewano na kwamba, nchi yake itaendelea na mazungumzo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!