Thursday, August 2, 2012

MANECK AJIBU TUHUMA ZA KUUZA BEAT


Producer wa AM Records, Manecky leo ameizungumzia kashfa inayomkabili ya kuwagonganisha wasanii wawili wa hip hop aliowapa beat moja.

Wasanii hao ni Izzo B na mwingine aitwaye Brian huku beat inayogombaniwa ikiwa ile ya wimbo wa Izzo B, ‘Mwaka Jana’.

Akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Manecky amekanusha kumuuzia beat Briain kwa shilingi laki 3 kama msanii huyo alivyosema jana na kwamba alimpa bure kwakuwa msanii huyo mara nyingi huenda kwenye studio hiyo na tayari amesharekodi nyimbo kadhaa kwenye studio hiyo.

Akielezea namna beat hiyo ilivyotengenezwa Manecky amesema kuna siku alienda Maisha Club ambako alikutana na wasanii kadhaa akiwemo Izzo na kuwasalimia. Anasema baada ya kuwasalia kuna mtu mmoja maarufu ambaye hakumtaja jina alimskia akimdiss kuwa yeye sio producer bali ni producer viduku.

Baada ya kuambiwa hivyo manecky ajisikia vibaya sana kuamua kuondoka kwenye club hiyo.

"Nilimaindi kiukweli, cha kufanya sikurudi hata home , nikaenda studio, na beat nikagongea pale, ile siku nakumbuka nilifanya beat kama tatu, moja wapo ikiwa ile, ambayo the same beat, kama baada ya siku mbili tatu , tukawa tumeitwa kwenye vikao vya Kili Music vile, nikampa Izzo. Na that beat natengeneza moyoni mwangu. akilini mwangu nilikuwa natengeneza beat kwaajili ya Izzo B.

Manecky anasema baadaye ndipo Brian alikuja kusikia ile beat na yeye akaipenda na kuifanyia wimbo kwa maana kwamba baadaye producer huyo angekuja kuweka vocal zake kwenye beat nyingine na tayari alikuwa amemwambia kuwa ile ni beat ya izzo.==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!