Wednesday, August 22, 2012

MARIA CAREY AMNUNIA NICK MINAJ BAADA YA KUSIKIA KUWA HUENDA AKAWA JAJI MPYA WA "AMERICAN IDOL"


Kuna tetesi kuwa Nicki Minaj anaweza kuwa jaji wa American Idol ijayo. Lakini kuna tatizo. 


Kama kweli first lady huyo wa Young Money akiungana na meza ya majaji wa shindano hilo la muziki, Mariah Carey anaweza akanuna siku nzima. 

Mariah Carey alichaguliwa kuwa jaji mpya wa American Idol kuziba pengo lililoachwa na Jennifer Lopez.

Inasemekana kuwa baada ya watayarishaji wa American Idol kumpigia simu Mariah ili kumpa taarifa kuwa wapo kwenye mazungumzo na Nicki Minaj kwaajili ya kuwa jaji mpya wa msimu wa 12 wa mashindano hayo, alichukia na kuamua kuikata simu. Hata hivyo litakuwa ni jambo la kushangaza kwa Mariah kuchukia wakati aliwahi kumshirikisha Nicki kwenye wimbo wake wa mwaka 2010 uitwao Up Out My Face.

Kwa sasa American Idol ambayo inatarajia kurudi tena mwezi January mwakani imegubikwa na ushindani mkali kutoka kwa show pinzani za “The Voice” na “The X-Factor”.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!