Sunday, August 5, 2012

MATUKIO YA KUKAMATWA KWA MAGARI YA MATANGAZO YA CHADEMA MOROGORO

Askari Polisi wa Kikosi cha Ulinzi wa Doria wanaotumia Pikipiki kwa jina la ‘ Chita’ ama ‘ Vodafasta’ wakilisindikiza Gari lenye namba T 747 ANJ aina ya Nissan Patrol baada ya kulikamata Jioni ya Augost 3, mwaka huu wakati wahamasishahi wake walipokuwa wakipita mitaani kuutangazia umma juu ya kufanyika kwa maandamano na mkutano wa kitaifa wa hadhara eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege , Manispaa ya Morogoro ambao ulipangwa ufanyike Augost 4, mwaka huu.

Mkuu wa Kituo Cha Usalama Barabarani Wilaya ya Morogoro aliongoza opapreshi ya kukamatwa kwa magari yaliyokuwa yakitumiwa na Chama hicho kupita mitaani kutangaza kufanyika kwa mkutano huo wakati Jeshi hilo likiwa limetoa amri ya kupiga marukufu kufanyika kwa maandamano na mkutano huo kutokana na sababu za kiusalama , kukamatwa kwa gari hilo na jingine namba T 622 CAY aina ya Ford Ranger ni baada ya kukaidi amri hiyo.

Hata hivyo majadiliano na mazungumzo kati ya Viongozi wa ngazi ya juu ya Jeshi la Polisi pamoja na wale wa Chadema ngazi ya kitaifa walifikia muafaka wa kusitishwa kwa mkutano huo na mandamano na Chama hicho kuruhusiwa kuendelea na mikutano yake Augoti 8, mwaka huu wakianzia Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa na Morogoro Mjini Augosti 18, mwaka huu, ambapo baadaye magari hayo yaliachiriwa pamoja na vijana kadhaa walliotiwa nguvuni.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!