Sunday, August 26, 2012

MAZUNGUMZO YA MALAWI NA TANZANIA KUHUSU MPAKA YAKWAMA


Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Malawi na Tanzania wamesema kuwa mazungumzo kati ya nchi mbili hizo kuhusu mgogoro wa mpaka yamemalizika bila mafanikio na kusisitiza kuwa mazungumzo hayo yataendelea ili kadhia hiyo ipatiwe ufumbuzi. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Ephraim Mganda Chiume amesema msimamo wa nchi yake ni kwamba, tatizo lililopo litatuliwe kupitia mazungumzo pekee.

 Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe amekiri kwamba kadhia yenyewe ni nzito lakini akaelezea imani yake kwamba itatatuliwa haraka iwezekanavyo. 

Malawi na Tanzania zimefanya mazungumzo kwa takriban wiki nzima kujadili suala hilo. Nchi mbili hizo zinazozana juu ya mpaka wa Ziwa Nyasa huku kila upande ukidai ziwa hilo ni sehemu ya ardhi yake.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!