Monday, August 27, 2012

MB DOG AJIPANGA KUJARIBU BAHATI YAKE KWENYE FILAMU


Hitmaker wa ‘Latifa’ Mbwana Mohammed aka MB Dogg ameamua kujaribu bahati yake kwenye tasnia ya filamu baada ya muziki kuonesha kumwelemea.

Mzee huyo wa nyimbo za malavidavi ataonekana kwenye filamu iitwayo ‘Nankonda wa Mikindani’. Filamu hiyo itaingia sokoni hivi karibuni.Mb Dogg amesema anashukuru jinsi watayarishaji wa filamu hiyo Dr. Cool Production walivyompa nafasi ya kuonesha uwezo wake kwenye uigizaji.

Katika filamu hiyo msanii huyo ameigiza kama main character na inadaiwa kuwa ameweza kuonesha uwezo mzuri licha ya kuwa hiyo ni filamu yake ya kwanza kuigiza.

Amesema mashabiki wake wa muziki wasubirie kuona kipaji chake kingine cha uigizaji na anaamini kuwa wataipenda filamu hiyo.

Katika kuonesha utofauti na filamu zingine, filamu hiyo imefanyika mkoani Mtwara.

Waigizaji wengine waliohusika ni pamoja na Uswege Mpepo, Dayana Nsumba, Pili Mlindiko na wengineo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!