Thursday, August 16, 2012

MESSAGE YA MKEO KWA JIRANI YAKO: "MPENZI NIMEKUMISS ILE MBAYA, NAOMBA HATA 5000 MAANA SINA KITU"......UNGEKUWA WEWE UNGEFANYAJE?


SWALI:
 wewe ni mwanaume umeoa kama miaka 8 iliyopita. Mmekuwa waaminifu ile mbaya kwenye ndoa yenu yaani mnaaminiana mpaka basi. 
 
Inatokea siku moja unashika simu ya mkeo unakutana na msg imeandikwa mambo ya kimapenzi like this! "Mpenzi nimekumiss ile mbaya, naomba hata elfu tano maana sina kitu kabisa,nijibu". mwisho wa kunukuu.

Ukiangalia namba ni ya mtu ambaye unamjua tena jirani yako, Unamuuliza wife anakurusha rusha baada ya kubanana nae kwa sana anakiri kuwa alikua na shida nayo hiyo elfu tano.
 
Ungekuwa wewe mwenzangu ungefanyaje?

 
 JAWABU   NA  USHAURI...
Asante sana kwa mail yako fupi lakini imebeba fundisho kubwa sana katika maisha yetu ya kimapenzi, mahusiano na ndoa. 
 
 Wakati naisoma mail hii nilikuwa  karibu na jirani yangu ambaye sitamtaja jina.Nilimuuliza hili swali  kupata mtazamo wake.Bahati nzuri  yeye alikuwa  ni victim.

Kabla sijawapa wasomaji  nafasi  ya kuchangia, naomba  nieleze  alosema  mama huyo.
 
**********************************************
 
 Kwa kweli tunaumia sana kwenye ndoa zetu siku hizi. Unajua mmeo anafanya kazi na hata kipato chake unakijua, lakini ukiomba hela kidogo kila siku yeye hana. 
 
Mimi mwenyewe haya yananiumiza sana. Mme wangu kila siku ukiomba hela hana hela.
 
 Kuna siku nililia sana. Nilikuwa nahitaji kama elfu 5 hivi. Mme wangu nilipomuomba hela akasema sina. 
 
Nilipompekua mfukoni, nilikuta kwenye Boxer ana laki 2 kazikunja, kwenye mfuko wa suruali ana kama laki na ishiri, kwenye mfuko wa shati ana kama elfu 50. Kwa kweli niliumia sana. Kumwibia siwezi, maana siyo tabia yangu.
 
Siku ya pili akawa amekaa kwenye kochi, alipoinuka akadondosha noti za elfu 50 zimekunjwa pamoja.
 
 Siyo siri, niliziokota nikakauka kabisa. Naye aliona haya hakuwahi kuniuliza hadi leo na shida yangu nikamaliza. 
 
Tatizo lake pia hataki kuona unasaidiwa na mtu, hasa wa jinsia nyingine. Kwa hiyo siku zote, huwa napata msaada kwa watu wengine, japo si kwa nia mbaya lakini huwa nahakikisha kwamba hajui kabisa.
 
Sasa kaka uliyetoa ujumbe hapo juu, inawezekana kabisa mkeo ni mwaminifu saaana. Tatizo liko kwako. 
 
Je, anapokuomba hela kama hiyo aliyoiomba kwa jirani yako huwa unamwambiaje? Inawezekana kabisa wewe ni chanzo kikubwa sana cha hali hiyo. 
 
Na alikurusha rusha kwa vile anajua unamjia juu. Chonde chonde kakangu, mjali mkeo.
 
 Mpe hela, kwani hiyo hela unatafuta kwa ajili ya nani? mama anatunzwa na baba,  kadhalika. Hivi, usipompa raha mwandani wako utampa nani tena!? 
 
Naomba usimwazie mabaya mkeo, ni hali ambayo hata wewe sikulaumu sana ila naomba tu ujirekebishe ili umpe raha mwandani wako. 
 
Mimi ni mwaminifu hadi leo, lakini kwa kuwa mme wangu nimejitahidi kumwelewesha na haelekei, na tena 
ukimwingizia issue ya hela hata kama mlikuwa mnacheka anabadilika.
 
Siku hizi nimeamua nimwache, ila nakopa kwa mtu na vile mimi nina vishughuli vyangu vinavyoniingizia kipato, nikipata narejesha kwa yule aliyenipa.
 
 Na unajua, sisi tulioolewa tunaogopa sana kutoa siri zetu za ndani kwa wanawake wenzetu, maana unahisi atamwambia X na Y. Unaona bora ukimwendela mwanaume siyo rahisi aseme.
 
Halafu nikutoe wasiwasi tena kuhusu neno MPENZI. Neno hili siku hizi linatumika ovyo sana. Inawezekana naye hana mipaka ya kulitumia. Usijikondeshe nalo. Inawezekana tu ni lugha ya mkeo kwa watu wote. Mchunguze kabla ya kumhukumu.
 
Nimeoandika mengi ila naomba uyasome utaokota mawili matatu.

Mama .........


KARIBUNI WAPENZI WASOMAJI  KWA MAONI
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!