Friday, August 3, 2012

Miss America atua Kenya Kukagua Miradi yake


Mrembo Wa Kimarekani anayeshikilia taji la Miss America kwa sasa Teresa Scanlan amewasili nchini Kenya jana asubuhi, na kuelekea eneo la Kipseo iliyo ukanda wa juu wa vilima vya Nandi, ambapo amekwenda kutembelea watoto ambao anawasaidia.


Miss huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa shirika la maendeleo la Imani ambalo ndio mdhamini mkuu, atatembelea baadhi ya familia, shule na baadhi ya wadau wakiwemo viongozi wa eneo hilo pamoja na waandishi wa habari.


Mrembo huyo ambaye kabla ya kushinda taji la Miss America alishinda taji la Miss Nebraska mwaka 2011 kabla ya kunyakua taji la Miss America mwaka uliofuata wa 2012.


Mrembo huyo ni balozi wa mashirika mengi ya kimataifa na safari yake ya Kenya ni mwendelezo wa kazi zake za kijamii.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!