Thursday, August 23, 2012

MISS PROGRESS INTERNATIONAL NAYE AKIMBILIA "BONGO MOVIE"


.
MISS Progress International 2010, Juliet William amegeukia sanaa ya uigizaji baada ya kumaliza mradi aliokuwa akiufanya wa kuwasaidia walemavu wa ngozi (albino).

Akiongea  na mwandishi wetu, Juliet alisema ameamua kuingia kwa asilimia mia moja kwenye gemu la uigizaji kwa vile amegundua ndiyo fani inayolipa hasa akizingatia kuwa ana kipaji.


Alisema kwa kuanzia anaandaa filamu yake inayokwenda kwa jina la Sister Juliet aliyomshirikisha Sylvia Shally.


“Nimeamua kujikita katika filamu kwa sasa, mradi wa kusaidia walemavu  wa ngozi nitaendelea nao baadaye. Kwa kuanzia nimeandaa filamu yangu ya Sister Juliet nikicheza na Sylvia Shally,”
alisema Juliet.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!