Thursday, August 2, 2012

Mrisho Ngasa Asema Hawezi Uzwa Kama GuniaMRISHO Khalfan Ngassa ameuzwa Simba kwa dau la Sh. Milioni 25 jana mchana, Azam imethibitisha.


Habari kutoka Azam,zimesema kwamba Simba wamelipa fedha hizo na wamesainiwa fomu za uhamisho na sasa Mrisho anafuata nyayo za baba yake Khalfan Ngassa, ambaye aliichezea Simba SC 1991/1992.Azam ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kudaiwa kubusu jezi ya Yanga baada ya kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Azam wamedai kumuuza mchezaji huyo kufuatia kushuka kwake kwa uwezo na kiwango chake kwenye soka.

Uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo. Inasemekana Mrisho Ngassa mwenyewe hajashirikishwa katika uhamisho na mpaka jana alipoulizwa alisema yeye hakuwa akifahamu chochote na yeye hawezi kuuzwa kama gunia japo mpira ndo kazi yake. 

Aliendelea kusema kwamba Azam hawajamtendea haki na hatakubali kwenda kuchezea timu ambayo hajashirikishwa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!