Friday, August 3, 2012

MRISHO NGASSA AANZA MAZOEZI SIMBA SC

 
Mrisho Ngassa akiwa mazoezini.
Gari aina ya Toyata Verossa  alilopatiwa Mrisho Ngassa.
 
Mrisho Ngassa pamoja na wachezaji wa Simba wakiwa mazoezi.
Mashabiki wakifuatilia mazoezi ya Simba.
Ngassa akiwa kwenye gari lake.
Wanahabari wakimhoji Ngassa.

KIUNGO mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa leo asubuhi ametua rasmi na kuanza mazoezi katika timu  yake mpya, Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba.


Ngassa alikuwa mmoja wa wachezaji wa Simba waliokuwa mazoezini kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Mashabiki kibao walijitokeza kumshuhudia kiungo huyo ambaye amejiunga Simba kwa kulipwa dau la Sh milioni 30 pamoja na gari aina ya Toyota Verossa lenye thamani ya Sh milioni 18.


Baadhi ya mashabiki waliokuja eneo la tukio ni vijana waliokuwa katika mlolongo wa kuwania kushinda shindano la muziki la BSS zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo.


Ngassa alionekana kuwa mwenyeji tu na alifanya mazoezi vizuri kwa ushirikiano na wenzake. Mazoezi hayo yalikuwa chini ya Kocha Msaidizi, Richaed Amatre raia wa Uganda.


Simba imeilipa Azam kitita cha Sh milioni 25 ili kumchukua Ngassa ambaye amekuwa akidai hana raha.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!