Thursday, August 2, 2012

MRISHO NGASSA AMALIZANA NA SIMBA - ALIPWA MILLIONI 30, GARI NA MSHAHARA WA MILLIONI 2 KWA MWEZI

Hatimaye leo mchana sakata la usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa akiichezea klabu ya Azam msimu uliopita, kabla ya jana kuuzwa kwenda klabu ya Simba limemalizika.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba, leo mchana walikutana na mchezaji mwenyewe ili kuweza kukubalina juu ya mahitaji yake binafsi, baada ya jana wekundu hao wa msimbazi kumalizana na Azam.

Kwenye mkataba wake mpya na Simba, Ngassa atapewa gari aina ya Verossa, ada ya usajili millioni 30 pamoja na kupewa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa kwenye klabu aliyotoka ya Azam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari mkataba ni mwaka mmoja.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!